May 17, 2016

MAYANJA
Klabu ya Simba imepanga kuliboresha benchi la ufundi kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kuleta makocha wenye uwaledi wa kukinoa kikosi chao.

Kauli hiyo, ilitolewa na Rais wa timu hiyo, Evans Aveva ikiwa ni siku chache tangu Simba walikose taji la Ubingwa kwenye msimu huu.

Akizungumza na Salehjembe, Aveva alikiri kuwepo kwa upungufu kwenye benchi hilo linaloongozwa na Mganda, Jackosn Mayanja huku akiahidi msimu ujao kuliboresha zaidi.

“Tunataka kwenye msimu ujao tuwe na benchi la ufundi litakalokidhi haja ya timu yetu, hivyo ni lazima tuliboreshe kuhakikisha tunafanya vema kwenye ligi kuu.


“Mfano kwenye mechi hizi za mwishoni za ligi kuu ikiwemo na Mwadui FC, utaona mchezo huo ulisimamiwa na kocha wa makipa, hiyo ni baada ya kukosa kocha msaidizi wakati kocha wetu Mayanja akitumikia adhabu ya kadi nyekundu,”alisema Aveva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV