May 18, 2016Katika kuhakikisha hawataki mchezo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, Ruvu Shooting imefunguka kuwa itafanya usajili wa nguvu kwa kusajili wachezaji saba watakaongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo.

Ruvu imepanda daraja msimu huu baada ya kushuka msimu uliopita kufuatia kufungwa na Stand United ambapo kulizuka utata lakini imerejea tena ligi kuu huku ikiwa haitaki kurudia makosa yaliyowasababisha washuke daraja.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema, kikosi chao kimeingia kambini Mei 9, mwaka huu na wameanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya huku wakitarajia kufanya usajili wa nguvu kwa kuleta majembe saba.

“Kocha anahitaji kuongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake katika nafasi ya kipa, mabeki namba mbili na namba nne, kiungo namba sita na nane, na washambuliaji namba tisa na 10.

“Wakati timu ikianza mazoezi ndipo mchakato wa usajili utakapoendelea kwa kusajili wachezaji mbalimbali na kuhusu kuacha wachezaji hilo litategemea na matakwa ya Kocha (Tom) Olaba kwani awali tulisajili wachezaji 24 hivyo kutufanya tuwe na nafasi zaidi ya kusajili,” alisema Bwire.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV