May 18, 2016


MEYA ISSAYA MWITA
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Issaya Mwita Charles naye ametoa ya moyoni kwa kuipongeza Klabu ya Yanga baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga inayonolewa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm, imefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mara ya pili mfululizo ambapo ubingwa huo ni wa 26 kwa klabu hiyo na kuifanya iweke rekodi ya kuwa klabu iliyotwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi nchini.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kutoka kwa meya huyo, ilisema kuwa kuendelea kufanya vyema kwa Yanga kwa kutwaa ubingwa huo kunaendelea kulipa sifa Jiji la Dar es Salaam.

“Niipongeze Yanga kwa kuweza kutwaa ubingwa wake kwa mara ya 26, tunafurahishwa na hili kwa kuwa mafanikio ya Yanga ni ya Jiji la Dar es Salaam nzima.

“Lakini nilikuwa nawatahadharisha kuwa wasiishie kwa kuonyesha kiwango tu walichonacho sasa, wanatakiwa kukazana zaidi hasa katika upande wa michuano ya kimataifa ambayo wanashiriki kwa sasa ambapo huko wanatakiwa kuongeza nguvu,” alisema meya huyo wa Dar.


Alisema anaitakia klabu hiyo maandalizi mema katika mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Sagrada Esperanca utakaopigwa leo Jumatano, Angola ambapo anaamini klabu hiyo itaweza kufanya vyema na kusonga mbele katika hatua ya makundi

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV