May 17, 2016


Simba wameamua kufanya usajili wao kwa umakini sana ili kuepuka mambo mengi na mojawapo ni hujuma.

Hivi karibuni, wachezaji wa kigeni akiwemo Hamisi Kiiza, Justuce Majabvi, Juuko Murshid, Vicent Agbani, Emiry Nimubona na Paul Kiongera waligoma kwa madai ya kucheleweshewa mshahara kwa siku tisa tu.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza, katika kikao maalum walichokaa viongozi wa Simba pamoja na wale wa kamati ya usajili, wamekubaliana kuangalia wachezaji ambao hawawezi kugeuka na kuwa sumu kwao.

“Unajua Simba ilikuwa na wachezaji wazuri sana, lakini baadaye walibadilika na kuwa sumu kwao. Sasa wanaona lazima wazidishe umakini.

“Hawaoni kuwa na mchezaji mwenye uwezo wa kufunga au kutoa pasi za mabao, lakini ndani ya timu anakuwa tatizo.

“Wanaona wachezaji nyoka wa namna hiyo ni tatizo kwa kuwa wanaweza kuwapandisha na siku inaguofuata wakawamaliza kabisa,” kilieleza chanzo.

“Hivyo sasa, Simba itakuwa makini sana ili kuepuka kuwa na watu ndani ya kikosi, kumbe wao ndiyo wanaoiangusha.”


Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alilalama kuhusiana na wachezaji waliokuwa wapenda fedha ndani ya kikosi hicho, waliwahujumu.

Hata hivyo, Hans Poppe hakuwataja wachezaji waliowajumu wakati wa msimu huu.

1 COMMENTS:

  1. Mchezaji kama Kiiza sio wa kuacha ila sio wa kutegemea. Timu kama SIMBA tunahitaji Kiiza wengi Kina Tabwe wengi ili mchezaji mmoja asijiona wa Maana. Tutamuona hana maana kesho ataonekana Dhahabu.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV