Wanachama wa Yanga wamecharuka na kufanya kitendo kinachoonyesha ni hasira kutokana na kuchana na kuchoma moto magazeti.
Wanachama hao wa Yanga, leo wamechoma moto magazeti ya Nipashena The Guardian katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani na Twiga, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Wanachama hao wamefanya hivyo wakipinga Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kusakamwa kw amakusudi na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
“Hii sasa imetosha, huyu Mengi na magazeti yake anamsakama Manji kila anapoona Yanga inafanya vizuri. Mara tu baada ya Yanga kutinga robo fainali hatua ya Kombe la Shirikisho, basi vyombo vyake vimeanza kuandika kwamba anatakiwa sijui kuondolewa Coco Beach.
“Hakuna asiyejua Manji amestaafu Quality Group, sasa anamtaja wa nini. Au anataka ashindwe kufanya kazi za Yanga kwa utulivu.
“Watuache, kweli tutatangaza watu wa Yanga waachane na kununua bidhaa zake,” alisema Abuu Chehekaheka.
Pamoja naye, wanachama wengine kama Edward Matiku, Clement Michael na Hashimu Mtanza nao walimuunga mkono pamoja na wengine waliokuwa pale kabla ya kuanza kuchoma moto magazeti hayo wakionyesha kuwa na jazba.
Hata walipoulizwa sababu kuu za kuchoma magazeti hayo yanayomilikiwa na Mengi, hakuna aliyetaka kujibu huku wakionyesha kuwa na jazba.
0 COMMENTS:
Post a Comment