June 13, 2016


MANJI
Chama cha soka mkoa wa Dar e salaam DRFA kimempongeza Yusuph Manji kwa kuchaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa klabu ya Young Africans kufuatia uchaguzi uliofanyika juni 11,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo amesema kitendo cha Manji kupata kura nyingi ni ishara tosha kwamba anakubalika na wanachama wa klabu hiyo licha ya kuwa hakuwa na mpinzani kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya mwenyekiti.

KASONGO
Kasongo amemuhakikishia Yusuph Manji  kuwa DRFA itaendeleza ushirikiano uliopo na uongozi wake pamoja na kamati nzima ya utendaji ya Yanga katika masuala mbalimbali ya kuendeleza soka la Dar es salaam.

Yusuph Manji  ameitetea tena nafasi hiyo kwa kupata kura 1,468 kati ya kura zote 1,470 zilizopigwa na kufufua tena matumaini ya wanachama na mashabiki wa Yanga.

Mbali na Manji, Kasongo amempongeza pia Clement Sanga kwa kurudi tena kwenye nafasi ya umakamu mwenyekiti baada ya kutangazwa mshindi kwa kupata kura 1,428.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV