June 28, 2016


Mashabiki wamewazidi nguvu na kuvunja geti la upande mmoja wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakilazimisha kuingia ndani ili kushuhudia mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe.

Hii ilitokea baada ya mashabiki hao kutakiwa kuondoka katika enero hilo kwa kuwa tayari idadi ya mashabiki kwenye Uwanja wa Taifa unaochukua mashabiki 60,000 ilikuwa imetosha. Kiingilio ni bure baada ya uongozi wa Yanga kupitisha hilo.

Jeshi la Polisi Tanzania limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wanaotaka kuingia kwenye Uwanja wa Taifa licha ya kwamba hakuna nafasi.


Tayari mageti yamefungwa, lakini mashabiki walitaka kuingia zaidi ya hapo licha ya maelekezo ya polisi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV