July 14, 2016


AS Roma ya Italia imeanza maandalizi yake ya msimu mpya wa Serie A kwa kushinda kwa mabao 16-0 dhidi ya  AC Pinzolo ambayo ni timu ya kawaida, yaani isiyo katika ligi ya kulipwa nchini Italia.

Katika mechi hiyo ya kirafiki, Edin Dzeko alipiga mabao manne, Mohamed Salah akapiga mawili na Diego Perotti na Juan Iturbe walikuwa kati ya waliopachika mabao.

AS Roma moja ya timu kubwa za Italia, ilibadili kikosi chote kipindi cha pili.

VIKOSI:
Kipindi cha Kwanza:
Alisson; Torosidis, Manolas, Zukanovic, Mario Rui; D'Urso, Paredes, Strootman; Salah, Dzeko, Perotti 

Kipindi cha Pili: 
Lobont; Emerson, Marchizza, Gyomber, Seck; Di Livio, Vainqueur, Gerson; Iturbe, Ponce, Ricci

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV