July 12, 2016


Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ amesema wachezaji wote wa kikosi hicho, wamepania kucheza mechi dhidi ya Medeama, Jumamosi.

Cannavaro kila mchezaji wa Yanga anataka ushindi katika mechi hiyo na mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwaunga mkono.

“Waje watuunge mkono, waje kwa wingi ili tupambane kwa niaba yao.

“Kweli kila mmoja anataka kushinda mechi hiyo. Itakuwa ngumu kwetu lakini tunataka kushinda na hakuna mjadala.”


Yanga inahitajika kushinda mechi hiyo ili kuhakikisha inaibua matumaini upya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV