July 12, 2016

GONZALEZ AKIWA NA JAFFAR IDDI

Baada ya kutema baadhi ya wachezaji waliokuwa wanafanya majaribio, makipa wawili Juan Jesus Gonzalez kutoka Hispania na Daniel Yeboah wanaendelea kupambana kupata nafasi.

Yeboah kutokea Ivory Coast na Gonzalez kila mmoja anataka nafasi ya kusajiliwa Azam FC.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema makipa hao wawili ni sehemu ya wachezaji wanaoondelea kufanya majaribio chini ya kocha kutoka Hispania na jopo lake.

YEBOAH
“Bado wanaendelea na mazoezi ambayo ni sehemu ya majaribio. Ikifikia wakati kama wamefuzu au la, taarifa itatolewa,” alisema Jaffar.

Azam FC imeamua kujiimarisha zaidi kikosi chake kuhakikisha inafanya kweli msimu ujao.

Lakini awali ilielezwa kwamba Yeboah, yeye alikuwa anakuja nchini kwa ajili ya kusaini. Hata hivyo, ujio wa Gonzalez unaweza ukawa umebadilisha hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV