July 4, 2016


Multichoice Tanzania imeonyesha namns ambavyo jamii inaweza kukumbukwa baada ya kutoa misaada kwa watoto yatima wa kituo cha Al Madina cha Tandale jijini Dar es Salaam, leo.

Timu nzima ya Multichoice Tanzania, ilitua katika kituo hicho ikiongozwa na Meneja Mtendaji, Maharage Chande na kupokewa na watoto hayo walioonekana kuufurahia ugeni huo.

Chande alisema kuanzia mwaka 2006 wamekuwa wakiwasaidia na wataendelea kuwa nao karibu.

“Februari mwaka huu, mkuu wa kituo hiki alileta mapendekezo yake kwetu. Sisi tumeamua kuyafanyia kazi siku chache kabla ya sikukuu,” alisema Chande.

Naye mlezi wa kituo hicho, Kuluthumu Yusuf alisema: "Nawashukuru sana Dstv kwa kuendelea kutusaidia, kutoa ni moyo na wanauonyesha kwetu. Tunaomba na makampuni mengine yaige mfano wao."

Kati ya zawadi zilizotolewa ni pamoja na mashuka, charahani, magodoro, sukari, mchele na vitu vingine mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.

Multichoice kupitia DSTv wamekuwa wakionyesha chaneli mbalimbali ambazo ni maarufu nchini na Afrika nzima kama SuperSport upande wa michezo, M net, Movie Magic na nyingine upande wa filamu lakini kuna zile maarufu za taarifa ya habari kama CNN, Al Jazeera, BBC na nyingine nyingi zinazohusisha elimu na burudani.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV