July 31, 2016

Kama ulikuwa inaamini Jerry Muro amefungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ujue umekosea.

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema hatambui lolote kuhusiana na kufungiwa kwa Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo kongwe zaidi nchini.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Manji amesema klabu hiyo inaendelea kumtambua Muro kama mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano na anaendelea kufanya kazi zake kama kawaida.

“Kama taarifa tumesikia kwenye magazeti na redio, kweli taasisi kama Yanga, msemaji wake anasimamishwa kwa njia hiyo.

“Hao waliomsimamisha pia ni taasisi, vipi wafanye hivyo. Yanga tunawezaje kuamini hilo? Muro bado yuko kazini na anaendelea na shughuli zake kama kawaida,” alisema Manji.

Manji amesisitiza, kuwa kama ni kweli basi TFF inapaswa kutoa hukumu ya kumfungia Muro kama ambavyo wamekuwa wakisikia.

TFF kupitia kamati ya nidhamu ilitangaza kumfungia Muro mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na kumpiga faini.

Lakini imekuwa ikisita kutoa hukumu yake inayohusiana na Muro, jambo ambalo linaifanya Yanga kuona kuna upotofu wa mambo na kukiukwa kwa usahihi.


Hukumu ya Muro imekuwa ni kitu cha uficho licha ya kamati hiyo chini ya TFF kumhukumu, jambo ambalo linaonekana ni kichekesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic