July 15, 2016


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuwa, kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo, wataanza zoezi la usajili wa wachezaji watakaoshiriki michuano ya vijana chini ya miaka 15 ya Airtel Rising Stars.

Msimu mpya wa michuano hiyo kwa mwaka huu ulizinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, jijini Dar es Salaam.

Timu zinazotarajiwa kushiriki kwa upande wa wavulana ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Mwanza na Morogoro huku za wasichana zikiwa ni Lindi, Zanzibar, Ilala, Temeke, Kinondoni na Arusha.

Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, amesema TFF kwa kushirikiana na Kampuni ya Airtel wana lengo moja la kuhakikisha soka la vijana linapiga hatua hapa nchini.

“Dhumuni letu ni kuona vijana nao wanapata fursa ya kuonyesha vipaji vyao, na tunataka miaka michache ijayo timu yetu ya taifa iundwe na wachezaji kutoka kwenye michuano hii kama ilivyo sasa hivi katika kikosi cha Serengeti Boys,” alisema Mwesigwa.


Naye, Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde, matarajio yao ni kuona msimu huu michuano hiyo inakuwa bora zaidi kuliko iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic