July 12, 2016Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara sasa amethibitisha atapelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu.

Manara anatarajia kuondoka kati ya Ijumaa au Jumamosi kwenda kwenye matibabu ya jicho.

Jicho la kushoto lake la kushoto limepata tatizo na halioni tena na lile la kulia, uwezo wake wa kuona umepungua kwa asilimia kubwa.

Manara amezungumza na SALEHJEMBE na kusema baada ya kuwa na chaguo kati ya Ujerumani, India na Uturuki, hatimaye amepata hospitali nchini India.


“Kweli natarajia kwenda India kwa ajili ya matibabu, ila nashukuru maumivu ya kichwa yamepungua. Ingawa jicho la kulia nalo limepunguza uwezo wa kuona hadi kufikia asilimia kumi tu,” alisema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV