January 16, 2021

 



KIUNGO wa Klabu ya Simba, Bernard Morison amesema kuwa maisha ya mpira sio vita bali ni kazi ndani ya uwanja hivyo kila kitu kwakwe anajifunza.

Nyota huyo aliibuka ndani ya kikosi cha Simba akitokea Yanga ambapo uhamisho wake umekuwa na vurugu nyingi hasa kufuatia mabosi wake wa zamani Yanga kudai kwamba bado ni mali yao.

Ndani ya Simba hajawa akionekana kikosi cha kwanza tofauti na alipokuwa Yanga ambapo mabosi wa Simba wameeleza kuwa ana matatizo ya kiafya ambayo yatamuweka nje kwa muda wa miezi sita.

Habari zinaeleza pia huenda ikawa mwisho kwa nyota huyo mpanda mpira kuwa na jezi za Simba kwa kuwa kuna ingizo jipya ambaye ni Perfect Chikwende ataziba nafasi yake.

Morrison amesema:-"Maisha ya mpira sio vita,watu wanapaswa waelewe kwamba nimeishi Yanga kwa furaha na sasa nipo ndani ya Simba maisha yanaendelea.

"Kikubwa ni kwamba kila sehemu kuna furaha na kila timu ni bora. Unaweza kusema kwamba ninaweza kusema vibaya kuhusu Yanga hapana hiyo sio sawa,tatizo wengi wanafikiria mabaya kule ambako ulikuwa," .

17 COMMENTS:

  1. Waeleze hao utopolo waache kukuroga maana wamezidi sasa

    ReplyDelete
  2. No vigumu sana kuamini lakini jamaa maumivu yake hayajulikani yalipoanzia Hawa watu Kama Kila siku jina la Morrison haliwatoki kwenye vinywa vyao hawashindwi kumfanyia Mambo ya kishirikina

    ReplyDelete
  3. Mpeleke kwa mama yako akampatie dawa ili asiwe anarogeka kama wewe ambavyo hirogeki mtoto wa mama

    ReplyDelete
  4. Kama wewe mama yako ni kigagula unadhani kila mtu kalelewa kichawi? Pelekeni hiko uchawi wenu utopolo ninyi

    ReplyDelete
  5. Ukishaona unawaza uchawi basi ujue una elements za hio kitu

    Morrison wa kaongea vzr tu sijui hizo stori za uchawi zinaingiaje apo

    Kwa lazima kuchangia kila makala. Sisi ni ndugu wakuu

    ReplyDelete
  6. Paka fc wamekurupuka kumsajili morrison, yanga ni wasomi bhana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna usomi mwingi nafikiri utakuwa unazungumzia usomi wa kutumia tunguli mpo vizuri sekta hiyo utopolo

      Delete
  7. Wamesomea wapi na fani ipi, ya umbea na ulozi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli Miiba ni Noma! Mahela yote yale waliyolipa Simba arafu mchezaji anaishia jukwaani kama shabiki wa kushangilia?

      Delete
  8. ATAPONA KAMA WALIVYOPONA WENGINE, KWANI UNADHANI YEYE HAJUI ALIPOJIKWAA? SIO MJINGA

    ReplyDelete
  9. Mapovu tuuu, hata mnajua Morrison anaumwa nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hatujaambiwa na Uongozi haujaweka wazi. Ila Manara kasema ni Miiba. Labda itakuwa ni mambo ya Giza. Mbwembwe nadhani ya ile picha wakati anasaini Simba SC ndio zimemsababishia. Ilitakiwa aondoke kimya kimya. Kumbuka Njohole alivyoshuka kwenye Gari ya Gulamali Uwanja wa Taifa sura yake ilionyesha woga na kwamba aliwakosea wana Msimbazi.

      Delete
  10. Kwa hiyo anaomba samahani yanga? Yanga hatuna roho mbaya mtu anaekuheshimu unamheshimu. Kama alikuwa anataka kuondoka angetuomba na wanaomuhitaji wangefuata taratibu Wala tusingechukia mbona makambo aliondoka vizuri na saizi baado tunamkaribisha nyumbani. Njoo utubu kwa baba zako yanga tutakusamehe na kukutemea mate ya baraka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic