July 12, 2016


Wapinzani wa Yanga katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho barani Afrika, Medeama ya Ghana, itawasili jijini Dar es Salaam, keshokutwa Alhamisi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).

Yanga watakuwa wenyeji wa Medeama katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumamosi kuanzia saa 10 jioni.

Huu ni mchezo wa tatu kwa Young Africans katika harakati za kuwania Kombe la shirikisho hatua ya makundi. Michezo miwili ya awali ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid Mansour.

Kamishna wa mchezo huo atakuwa Pasipononga Liwewe kutoka Zambia na maofisa wasimamizi ni Mfubusa Bernard ambaye atasimamia utendaji wa waamuzi wakati Mratibu Mkuu wa mchezo huo kutoka CAF atakuwa Ian Peter Keith Mc Leod.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic