July 13, 2016


Wanachama na mashabiki wa Yanga, wametua nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara na kukabidhi mchango wao kwa ajili ya matibabu.

Pamoja na Wanayanga hao kutoa mchango wa Sh 1,055,000 lakini bado Manara amewaambia akitoka kwenye matibabu nchini India, kazi wanayo.

“Ninawashukuru sana, huu ndiyo utani wa Simba na Yanga uliokuwepo enzi zile. Upinzani lakini undugu wa kweli haukufa.

“Lakini niwaambie, nikirudi kutoka India nitakuwa fiti. Kazi kwenu, si mnajua mimi na Yanga ni mbingu na ardhi,” alisema Manara na kuwachekesha wageni wake.

Wanayanga hao walichanga fedha hizo kupitia makundi mbalimbali ya mitandao ya Wanayanga.

Manara anatarajia kuondoka nchini Jumamosi kwenye nchini India kwa ajili ya matibabu.Awali, mara tu baada ya kuwapokea mchango, aliwaambia hivi: “Nashukuru sana wenzangu, mchango huu mnaweza kuuona ni mdogo sana. Lakini ni mkubwa sana kwa kuwa gharama ni kubwa sana.

“Nyie sasa mmredusha zile enzi za Yanga na Simba ambao walikuwa wakiishi undugu wa enzi zile. Msiba wa Yanga wanazika Simba, Yanga wanazika Simba. Hivyo ni jambo zuri sana,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV