July 13, 2016


Kila mtu anakuwa na nafasi anapokuwa ofisini kwake. Uthibitisho ni picha hii, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa akimpa maoni yake baada ya kuamua kwenda kushuhudia mazoezi ya Yanga.


Jiulize, kama Mwambusi anegkuwa amekwenda ofisini kwa Mwigulu ambaye anapigiwa saluti hadi na IGP, angeweza kuweka pozi hilo? Ndiyo maana unaambiwa, kila mtu na ofisini kwake bana! Hii ndiyo picha ya siku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV