July 12, 2016


Wakuu wawili wa mawasiliano wa Yanga na Simba, jana walikutana na kuonyesha wanavyoweza kuishi nje ya kazi yao.

Muro ambaye ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano na habari katika klabu ya Yanga kama ilivyo kwa Manara upande wa Simba, walionyeshana upendo kwa kuzungumza huku wakitaniana.

Wawili hao walikutana wakati wa kuuaga mwili wa mwandishi mwandamizi wa michezo wa gazeti la Majira, Elizabeth Mayemba.

Shughuli hiyo ilifanyika Tabata jijini Dar es Salaam, jana na Muro na Manara waliongozana wakiwa wameshikana mikono.

Hata baada ya kuaga, walionekana wakiwa wameshikana mikono na kubadilishana mawazo kuhu wakisababisha watu wengi kuwazunguka.


Utani ulitawala kwa kiasi kikubwa hadi baadhi ya waliokuwa katika enero hilo wote kukimbilia walipokuwepo wawili hao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV