July 12, 2016


Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la kumsaka Miss Tabata 2016 litafanyika Julai 22 kwenye Ukumbi wa Da West Park, Tabata.

Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema jana kuwa warembo 38 wanaendelea na mazoezi kujiandaa na shindano hilo linaloandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment.

Kapinga alisema kuwa watafanya mchujo na kubaki na warembo 16 tu watakaopanda jukwaani.

Warembo wanaoendelea na mazoezi chini ya wakufunzi Neema Mchaki, Bokilo na Pasilida Bandali ni Happiness Paul (21), Neema Makwaia (21), Rose Lucas (22), Mariam Maabadi 23), Sabrina Khalifa (20), Catherine Alex (22) na Grace Malikita (21).

Wengine ni Rachel George (21), Nasra Munna (23), Jackline Evarest (21), Flora Msigwa (21), Akiza Mugashe (21), Neena Linus (21), Noela Pastory (21), Neema Zablon (24),  Narcisa Wilbert (19) na Jesca Jackson (22).

Pia wamo Latipha Dibwe (18), Salma Abeid (19), Fatma Mapunda (22), Dinnah David (24), Joyce Kweka (22),  Jesca Daniel  (22), Happiness Mnyeke (20),  Grace Matiko (19), Olanda Lifilima (21), Joyce Nyimbo (23), Zena Bakari (17), Sylvia Weru (20), Esther Ikwabe (20), Tamika Mwakitalu (23), Fides Fredson (22), Sharifa Ally (23), Monica Massory (21), Veronica Godfrey (21) na Rahma Huwel (24).

Naye Mkurugenzi wa shindano hilo ambaye pia ni mkuu wa kambi, Godfrey Kalinga alisema warembo watakaoshiriki kwenye fainali watatembelea mbuga za wanyama ili kupromoti utalii wa ndani. Alisema, washiriki watano watakaoshika nafasi za juu watashiriki kwenye shindano la Kanda ya Ilala ‘Miss Ilala’, na baadaye Miss Tanzania.

Miss Tabata inaandaliwa na Keen Arts ambayo ni kampuni tanzu ya Bob Entertainment wakati Ambasia Mallya ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.

Miss Tabata inadhaminiwa na Lete Raha, DataStar College, Global Publishers, CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti5 Kitwe General Traders na Bob Entertainment.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV