July 13, 2016Mshambuliaji Ibrahima Fofana kutoka nchini Ivory Coast ametua nchini mchana huu kufanya majaribio ya kujiunga na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC.

Fofana mwenye umri wa miaka 26, ametua akitokea timu ya Union Sportive de Ben Guerdane ya Tunisia aliyokuwa akiichezea msimu uliopita uliomalizika Juni 14 mwaka huu, aliyojiunga nayo akitokea kikosi cha Asec Mimosas ya Ivory Coast alikodumu tokea mwaka 2013-2015.


Hata hivyo, Fofana atapumzika kabla ya kuanza majaribio chini ya jopo la makocha kutoka Hispania ambao wamekuwa wakiwajaribu wachezaji kadhaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV