July 13, 2016


Aliyewahi kuwa mtangazaji wa michezo na habari nyingine katika Shirika la Habari la BBC kupitia Idhaa ya Kiswahili, Hafsa Mossi ameuwawa kwa kupigwa risasi.

Hafsa ambaye alikuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura, leo.


Mtandao wa BBC umesema Hafsa aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.

Msemaji wa rais wa Burundi, Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV