Kampuni ya Acacia Gold Mine ya Bulyanhulu mkoani Shinyanga imevunja mkataba wake mnono zaidi na klabu ya Stand United.
Stand United ndiyo ilikuwa klabu ya yenye mdhamini mwenye udhamini mnono zaidi kwa kuwa ilikuwa ikiingiza hadi kitita hadi Sh bilioni 1.2.
Lakini Acacia imeamua kuvunja mkataba wa takribani miaka miwili iliyobaki kutokana na vurugu kubwa ndani ya klabu hiyo hasa baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuamua kuwatambua viongozi wengine ambao hawakuwa madarakani awali.
Waanzilishi wa klabu hiyo walikuwa ni makondakta wa stendi ya mkoa wa Shinyanga, lakini baada ya kuonekana kuna udhamini, watu wengine wakajitokeza na kupewa sapoti kubwa na baadhi ya viongozi wa juu wa soka.
Kutokana na hali hiyo, Acacia imeamua kujitoa ili kukwepa migogoro hiyo, hali ambayo sasa itakuwa mzigo kwa walioichukua timu na huenda itakuwa kazi ngumu kwao kuiendesha kama walivyotarajia.
0 COMMENTS:
Post a Comment