TANDAU |
Kongamano maalum kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali linatarajiwa kufanyika Jumamosi jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo litafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na wadau mbalimbali watakutana kujadili masuala ya soka.
Mratibu wa Kongamano hilo, Henry Tandau amesema Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ndiye atakuwa mgeni rasmi.
“Kongamano litafanyika kwa siku mbili na ajenda ya kwanza ambayo tutaanza nayo itakuwa ni Uongozi na Utawala Bora,” alisema Tandau na kuongeza.
“Lengo kabisa ni kuchangia mawazo kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa soka kupitia kutatua matatizo yaliyopo.”
Alisema kongamano hilo litakuwa linaendelea na kingine itakuwa ni kulifanya kuwa rasmi kwa lengo la kusaidia michezo nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment