August 14, 2016


Neymar amefunga bao na kuisaidia Brazil kuitwanga Colombia kwa mabao 2-0 na kutinga nusu fainali ya Michezo ya Olompiki inayofanyika Rio nchini Brazil.

Neymar ambaye ni nanodha wa Brazil alifunga bao hilo safi kwa mkwaju wa adhabu.

Wakati fulani mechi hiyo ilisimama baada ya Neymar kumkwatua kwa makusudi mchezaji wa Colombia. Mwamuzi akamlamba kadi ya njano la wenzake hawakubali wakataka kumchakaza Neymar, jambo ambalo lilizua tafrani kubwa.

Brazil lianza kwa kusuasua na kuwafanya mashabiki wake kuanza kuwazomea wachezaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV