August 5, 2016


Kikosi cha Simba, kimeendelea na mazoezi leo huku kikifanya jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kabisa baada ya kumaliza kambi yake ya mjini Morogoro.

Chini ya Kocha Joseph Omog, Simba imefanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam, leo.

Mashabiki wengi wamejitokeza kukiangalia kikosi hicho kinachojiandaa na mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa msimu huu kitakapoivaa AFC Leopards ya Kenya katika mechi ya kirafiki katika Simba Day itakayopigwa, Jumatatu ambayo ni siku ya Nane Nane.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV