August 5, 2016


Mshambuliaji mpya wa Simba, Laudit Mavugo amekata kiu kabisa kuhusiana na ile filamu yake ya anakuja haji. Na leo ameanza mazoezi rasmi akiwa na timu hiyo.

Mavugo raia wa Burundi, ameungana na Kikosi cha Simba ambacho kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwa ni mara yake ya kwanza, Mavugo alionekana ni kama mwenyeji, asiye na woga na aliyechangamka hivyo kumfanya awe ni mwenye furaja muda mwingi.

Mshambuliaji huyo anatokea Vital'O ya Burundi na amekuwa gumzo msimu wa pili sasa, kwamba anatua Simba lakini mwisho mashabiki na wanachama wa Simba waliishia kumuona kwenye picha tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV