August 16, 2016


Pamoja na kwamba Diego Coasta aliisaidia Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England, msimu huu, lakini wakati mwingine anakuwa kama mwendawazimu.

Costa raia wa Hispania anapenda ubabe hata sehemu yenye utulivu au ambako hakuna sababu ya ubabe.

Mfano katika mechi hiyo waliyoshinda, alimkanya kipa wa West Ham United, Adrian nusura amvunje mguu.

Mazingira, hayakuwa yakionyesha kwamba alivyokwenda lazima angefanya hivyo. Lakini alionekana kulenga kwa makusudi kabisa kumuumiza.

Hata kama ndiyo ametokea Brazil Uswahilini, braza huyu naye kazini. Eeh!
2 COMMENTS:

  1. sio mwehu anacheza chini ya uangalizi wa refa. kama marefa wa epl hawachukui hongo ni nini zaidi. karibu kila mechi huyu costa anapostahili kadi nyekundu analelewa na marefa. hii foul peke yake ilistahili kadi nyekundu .lakini hajapewa hata njano. msije mkashangaa tajiri wa chelsea akaja filisika. n wewe mwandishi wetu mbumbu hua kazi yako kumsifia

    ReplyDelete
  2. sasa hii story uliotuandikia mwamuzi alikua wapi .au ilikua baa hii?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV