August 15, 2016

ZEBEN NA MSAIDIZI WAKE
Kocha Mkuu wa Azam, Mhispania, Zeben Hernandez, amesema kikosi chake kipo vizuri katika kila idara, isipokuwa kwenye eneo la ushambuliaji ambacho hakijafikia kiwango anachotaka.


Wikiendi Zeben iliyopita alikishuhudia kikosi chake kikilazimishwa sare ya bao 1-1 na URA ya Uganda katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi, Dar Ijumaa iliyopita. Mchezo huo ulikuwa wa pili kwa Azam kutoka sare baada ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting ya Pwani.

Katika mechi zake, Azam inaonekana kumkosa vilivyo straika Kipre Tchetche ambaye aliuzwa nchini Oman.
Zeben amesema kuwa safu yake ya ushambuliaji ndiyo inayomuumiza kichwa mpaka sasa kutokana na kutokuwa fiti kwa kushindwa kufunga mabao kwenye nafasi ambazo wanazitengeneza.

“Tupo tayari kwa mapambano ya ligi pamoja na mchezo wetu ujao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga lakini tuna dosari kidogo kwenye nafasi ya ushambuliaji ambapo wanahitaji marekebisho kidogo ili kuwa katika kiwango kile ambacho mimi nakitaka.

“Siyo kwamba ni wabaya kabisa, hilo hapana, ila wanachokosea ni kutokuwa siriazi kwenye kumalizia nafasi zile ambazo tunakuwa tunazitengeneza na mechi hizi mbili zilizopita ni ushahidi tosha lakini nitawapa mazoezi ya kuwafanya kuwa bora zaidi kabla ya kuanza kwa ligi,” alisema Zeben.


Azam kwa sasa ina washambuliaji John Bocco na Mzimbabwe, Bruce Kangwa mara baada ya kuachana na washambuliaji wake Didier Kavumbagu, Allan Wanga (wameachwa) sambamba na Tchetche aliyetimkia timu ya Al Nahdha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic