Kocha Mkuu wa Azam, Mhispania, Zeben Hernandez, amesema kwamba kikosi hicho kinahitaji marekebisho machache kabla ya kuanza kucheza aina ya soka ambalo amekuwa akilitaka kuona linachezwa na timu yake.
Zeben ambaye amepokea kijiti cha Muingereza, Stewart Hall katika kukinoa kikosi hicho mpaka sasa ameshakiongoza kushika usukani wa ligi kikiongoza kikiwa na pointi nne kikipishana na Simba kwa idadi ya mabao ya kufungwa na kufunga.
Zeben amesema kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kuwanoa wachezaji wa maeneo ya ulinzi na ushambuliaji ambapo ndipo wameonyesha wanahitaji marekebisho kwa ajili ya kuendana na aina ya soka analolihitaji.
“Tayari nimeshaanza kuona mwanga ndani ya timu ambapo wachezaji wameonyesha wanaelewa mbinu zangu ninazowapa ila tatizo limebaki kwenye nafasi za ulinzi na washambuliaji ambapo napo wakishika mifumo ninayofundisha basi tutakuwa moto sana.
“Nadhani sitachukua muda mrefu kuwaona wanacheza namna navyotaka kwa sababu ni sehemu ndogo tu wamebakiza kabla ya kuwa sahihi na kucheza vile ambavyo mimi nataka kuwaona wanacheza,” alisema Zeben.
0 COMMENTS:
Post a Comment