August 2, 2016Kuna taarifa zilizotufikia punde zinaeleza bilionea kijana Mohammed Dewji, amekubali kuipa Simba fedha zitakazoisaidia kufanya usajili.


Bado haijajulikana atatoa kitita cha kiasi gani lakini taarifa zinasema, Dewji maarufu kama Mo atatangaza kiasi atakachotoa leo.

Jana, uongozi wa Simba ulimuandikia barua kumuomba Mo atoe fedha za usajili kama alivyoahidi kusaidia wakati akitangaza nia yake ya kutaka kununua asilimia 51 za klabu ya Simba.

"Kuna uwezekano atatoa hadi zaidi ya Sh milioni 80, lakini hatujajua, ila taarifa zinasema Mo amekubali kutoa fedha hizo," kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV