August 23, 2016



Wachezaji wanakumbatiana, wanapeana mikono.
 
Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza mchezo.

Dakika ya 90 + 2: Mazembe wanapoteza muda kwa kupiga pasi na kuchelewa kucheza mipira iliyotoka.

Dakika ya 90: Dida anapangua shuti kali kutoka nje ya 18, inakuwa kona.

Dakika ya 90: Zimeongezwa dakika 3.

Dakika ya 89: Mazembe wanalishambulia lango la Yanga. Dida anafanya kazi nzuri kwa kupangua shuti kali linalotoka nje.

Dakika ya 87: Mazembe wanapiga faulo lakini inakuwa haina makali, Yanga wanaokoa.

Dakika ya 86: yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kaseke anaingia Matheo.

Dakika ya 86: Mazembe wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Yanga.
 
Dakika ya 81: Mahadhi na Niyonzima wanapigiana pasi lakini wanashindwa kuipennya ngome ya Mazembe.
 
Dakika ya 79: Yanga wanaonyesha bado wana uhai wa kupambana.
 
Dakika ya 74: Yanga wanapata bao la kwanza baada ya mpira wa faulo aliopuga Haruna Niyonzima kugonga mwamba wa juu kisha Amiss Tambwe akaumalizia wavuni. Mazembe 3, Yanga 1.
 
Dakika ya 71: Mahadhi anaingia na mpira anatoa pasi nzuri lakini inatolewa na kuwa kona ambayop haikuzaa matunda.

Dakika ya 68: Anaingia Mahadhi anatoka Msuva.
 
Dakika ya 66: Yanga wanapata faulo, anapiga Niyonzima lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 63: Kalaba anaipatia Mazembe bao la tatu baada ya kumpiga chenga Dida baada ya uzembe wa mabeki kisha kufunga kwa urahisi.

Dakika ya 62: Mchezo umeendelea baada ya Mpangi kupatiwa matibu na kuendelea kucheza.

Dakika ya 60: Mchezo umesimama kwa muda, kutokana na mchezaji wa TP Mazembe kuumia, ni Jonathan Mpangi.

Lilipigwa shuti kali kutoka kulia, Dida akalipangua lakini hakukuwa na beki wa Yanga aliyekuwa karibu kuokoa jahazi, ndipo Kalaba akamalizia kiulaini. Mazembe 2- Yanga hawajapata kitu.

Dakika ya 54: TP Mazembe wanapata bao la pili kupitia kwa Rainford Kalaba ambaye alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na winga wake kutoka kulia.

Dakika ya 52: TP Mazembe wanafanya shambulizi la nguvu na kukosa nafasi ya wazi, kipa wa Yanga, Dida anafanya kazi nzuri ya kuokoa hatari.

Dakika ya 50: Yanga wamemiliki mpira muda mwingi lakini wanacheza kwenye eneo lao zaidi.

Dakika ya 47: Yanga wanaonekana kutokuwa na papara licha ya kuwa pungufu na wapo nyuma kwa bao  1-0.
 
Dakika 45: Kipindi cha pili kimeanza matokeo ni 1-0, wenyeji wanaongoza.

Timu ndiyo zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili, Yanga ameanza kutoka Kocha Hans van Pluijm.


MSIMAMO ULIVYO KATIKA KUNDI A


P     W      D       L     GF     GA     Pts

1. TP Mazembe   5       3       1       1       7       4       10

2. Medeama        5       2       2       1       8       7       8

3. Mo Bejaia       5        1       2       2       1       2       5

4. Yanga             5       1       1       3       3       6       4



Mwamuzi anapuliza kipenga kuonyesha kuwa ni mapumziko

Dakika 45 + 2: Muda wowote mchezo utakuwa ni mapumziko

Zimeongezwa dakika mbili.

Dakika ya 45: bado matokeo ni 1-0

Dakika ya 42: Yanga wapo nyuma kwa bao 1-0.

Dakika ya 30: Beki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ ametolewa nje kwa kupewa kadi nyekundu kutoka na kucheza faulo.


Kikosi kinachoanza cha Yanga kinachoanza hiki hapa:
Deo Munishi
Hassan Kessy
Mwinyi Haji
Andrew Vincent
Mbuyu Twite
Juma Makapu
Simon Msuva
Thabani Kamusoko
Amissi Tambwe
Deus Kaseke
Haruna Niyonzima

WALIOPO BENCHI
Beno Kakolanya
Oscar Joshua
Pato Ngonyani
Juma Mahadhi
Mateo Anthony


Huu ni mchezo wa Kundi A katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga haina nafasi ya kusonga mbele wakati tayari  TP Mazembe imeshajihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali ya Shirikisho, ila ushindi leo utawawezesha kuongoza kundi hilo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic