September 24, 2016Bondia maarufu nchini, Francis Cheka ameibuka katika mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Cheka aliwashitua mashabiki waliokuwa uwanjani hapo, hawakutegemea kumuona hasa ikizingatiwa ni mkazi wa Morogoro.

Bondia huyo, alishuhudia mazoezi hayo, baadaye akazungumza na Mussa Hassan Mgosi ambaye ni rafiki yake.

Cheka ambaye ni shabiki wa Mnyama alionekana ni mwenye furaha aliyeridhishwa na mazoezi kikosi hicho chini ya Makocha, Joseph Omog na msaidizi wake, Jackson Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV