September 1, 2016

MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI YA SIMBA, ZACHARIA HANS POPPE.
Shirikisho la Soka la Kimataifa(Fifa), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwamo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukisema mameneja wote wa usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) hawana budi kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa mbalimbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.

FIFA limeleta mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine lakini kabla ya kufanya hivyo utasaidia kupata taarifa kamili za mchezaji huyo na shabaha kuu ni kurahisisha mawasiliano ya TMS Managers nchi nzima, klabu na mashirikisho mbalimbali duniani.

GPX ni kama mtandao wa kijamii unaoweza kulinganishwa na ‘WhatsApp’ unaofanya kuwa na mawasiliano ya karibu na FIFA imeagiza kuwa ni lazima mameneja wa TMS wa kila klabu na mashirikisho ya ya mpira wa miguu kujiunga na mtandao huo ambao si tu kwamba utafanya kazi katika nchi husika, bali pia unaunganisha ulimwengu wote.


Kwa mameneja wa usajili wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) watakaokuwa tayari basi hawana budi kuwasiliana na Meneja Usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupata maelezo ya kina ya namna ya kujiunga na mtandao wa GPX.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic