September 14, 2016

Kikosi cha Manchester United kimesafiri leo kwenda Uholanzi kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Europa League dhidi ya Feyenoord, mchezo utakaochezwa kesho Alhamisi.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho amewaacha mastaa kadhaa katika safari hiyo katika kile kinachoonekana kuwapumzisha.
  

Baadhi ya wachezaji hao wamo mastaa akiwemo nahosha wa timu hiyo, Wayne Rooney, wengine walioachwa ni Luke Shaw, Antonio Valencia na Jesse Lingard.

Wachezaji waliosafiri na timu kwenda Uholanzi ni:

Makipa:
De Gea, Romero, Johnstone.

Mabeki:
Darmian, Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Rojo, Smalling

Viungo:
Carrick, Fellaini, Herrera, Mata, Memphis, Pogba, Schneiderlin, Young.
Washambuliaji:
Ibrahimovic, Martial, Rashford.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV