September 14, 2016

Mshambuliaji Mtanzania ambaye anaichezea Genk ya Ubelgiji, licha ya kuwa bize na masuala ya timu yake hiyo ya Ulaya bado ameonyesha kuwa anaendelea kuwa mmoja wa Watanzania ambao wanafuatilia masuala ya nyumbani kwao baada ya kutoa pole kwa waathirika wa tetemeko la ardhi.
 





Samatta ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba na TP Mazembe ametumia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii kuelezea hisia zake juu ya tukio hilo lililotokea siku chache zilizopita mkoani Kagera na maeneo ya Kanda ya Ziwa kuelezea alivyoumia.

Akitumia taswira ya katuni anayemwaga machozi, Samatta aliandika:

“Poleni wakazi wa Bukoba, kwa kupoteza ndugu pamoja na mali kutokana na tetemeko la ardhi Mungu awatie nguvu na pia tuwaombee waliotangulia.”

  



Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, amekuwa na mwendelezo mzuri wa kucheza katika timu hiyo ambayo inatarajiwa kushiriki katika michuano ya Europa hatua ya makundi inayoanza kesho Alhamisi, Genk ikiwa ugenini kucheza dhidi ya SK Rapid Wien kwenye Uwanja wa Allianz.

Katika tetemeko hilo watu kadhaa walipoteza maisha, wengine wakijeruhiwa huku nyumba na miondombinu kadhaa zikiharibika, hali iliyosababisha Serikali kuwa mstari wa mbele kusaidia waathirika wote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic