September 14, 2016

Ilibaki kidogo staa wa Barcelona, Neymar asaini kwa matajiri wa Ufaransa, PSG kwa kitita cha pauni milioni 42, kabla ya kuitosa ofa hiyo na kuamua kusalia Barcelona kwa mkataba mpya wa miaka mitano.

Mipango hiyo ilikuwa ikifanywa kimyakimya katika dirisha la usajili lililofungwa hivi karibuni, vikao vya dili hilo vikimuhusisha Neymar, baba yake na Rais wa Klabu ya PSG, Nasser Al-Khelaifi.



 Kikao cha kwanza kilifanyika huko Ibiza, Hispania na Neymar akawekewa mezani ofa ya kitita cha usajili wa pauni 42m, kukodishiwa ndege anapokuwa na safari za mechi za Brazil pamoja na kuingia kwenye shea ya baadhi ya hoteli za matajiri hao.



Pamoja na yote hayo lakini dili hilo lilikufa katika kikao chao cha pili kilichofanyika Sao Paulo, Brazil na Neymar kuamua kuongeza mkataba wa miaka mitano wa kusalia Camp Nou.


Wakala wa Neymar, Wagner Ribeiro amenukuliwa akisema: “Al-Khelaifi alitoa mpaka ofa ya kushughulikia masuala yote ya ushuru wa Neymar atakapokuwa Ufaransa na akamuahidi kuwa mchezaji namba moja wa timu kitu ambacho hawezi kukipata akiwa Barcelona.


“Kulingana na ofa aliyopewa yeye ndiye angekuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani lakini ameamua kubaki Barca kwa kuwa ana furaha akiwa hapo. Nilimtaka aende PSG lakini baba yake alimshauri kubaki Barca.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic