September 22, 2016


Kikosi cha timu ya taifa ya vijana, Serengeti Boys imepaa kwenda Kigali, Rwanda ambako itaweka kambi kujiandaa na mechi yao dhidi ya Kongo.

Serengeti Boys inajiandaa mechi ya pili kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Wakongo hao ambao walilala kwa mabao 3-2 jijini Dar es Salaam.

"Timu imeondoka saa 3.00 asubuhi kwenda Kigali, Rwanda. Itafika saa 4.30 asubuhi kwa mujibu wa ratiba," alisema Alfred Lucas Mapunda, Msemaji wa TFF.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV