October 23, 2016


Na Hamisi Dauda, Bukoba
Mashabiki wa Yanga mkoani hapa, wameitaka Yanga kuendeleza dozi kama waliyoitoa kwa Kagera Sugar kwa timu nyingine.

Mashabiki hao, wamezungumza na SALEHJEMBE na kusema, wanaamini Yanga ina uwezo wa kushinda zaidi baada ya soka la kuvutia waliloonyesha na kuicharaza Kagera kwa mabao 6-2.


“Mabao sita kwa Kagera si kitu kidogo, hata sisi tunajua Kagera ni timu bora kabisa. Lakini Yanga imeonyesha kiwango kizuri sana na ikiendeleze,” alisema mmoja wa mashabiki hao baada ya mechi na kushangiliwa na wenzake.


Wengine walisisitiza wachezaji kutojihusisha na malumbano yanayoendelea klabuni na badala yake wafanye kazi yao kama kawaida ili wahakikishe wanaendelea kushinda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV