October 23, 2016


Simba imekuwa klabu pekee ya Tanzania, mashabiki wake kuendelea kuonyesha upendo kwa mmoja wa wachezaji wao ambaye alifariki dunia bado akiwa kazini.

Mutesa Mafisango raia wa DR Congo, alifariki dunia kwa ajali ya gari akiwa bado mchezaji wa Simba ambao wameendelea kuonyesha kuukumbuka mchango wake.

Mfano mzuri ni moja ya bango ambalo mashabiki wamekuwa wakiingia nalo uwanjani lenye picha ya mchezaji huyo.

Mara nyingine, wachezaji wa Simba hasa Shiza Kichuya, iwapo atafunga amekuwa akikimbilia kwenda kushangilia mbele ya bango hilo.


PUMZIKA KWA AMANI MAFISANGO.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV