October 7, 2016

NGASSA

Baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Toto Africans, Rogasian Kaijage kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, uongozi wa Toto umemkabidhi mikoba hiyo kwa muda Khalifani Ngassa ili kusaidiana na Wajerumani waliopo katika benchi la ufundi la timu hiyo kabla ya kupata kocha mkuu mpya.

Katika michezo saba ambayo Kaijage aliiongoza timu hiyo, Toto imeshinda mechi moja, sare mbili na kufungwa mechi nne jambo ambalo liliinua hasira za mashabiki wa timu hiyo na kumlazimisha ajiuzulu kuinoa timu hiyo.

Kuhusu suala hilo la Khalfani ambaye ni baba mzazi wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa, Mwenyekiti wa Toto, Godwin Aiko alisema: “Ni kweli tumeamua kumchagua Khalfani kuwa kocha wa muda.”

Alipotafutwa Khalfani alisema: “Kweli lakini mimi nitakuwa kocha wa muda tu wakati mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV