October 5, 2016

BOSSOU AKIPAMBANA NA LAUDIT MAVUGO RAIA WA BURUNDI
Beki wa kimataifa wa Yanga, Mtogo, Vincent Bossou, ameweka bayana kwamba kwa sasa haoni straika wa kumsumbua wala anayemtisha kukutana naye baada ya kumzima kirahisi mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo ambaye alisema kwamba angeisumbua ngome yao.

Mtogo huyo ambaye anaunda ukuta imara wa kikosi hicho akishirikiana na Andrew Vicent ‘Dante’, mpaka sasa wameweka rekodi ya kuwa timu iliyoruhusu mabao machache zaidi (mawili tu) kuliko timu nyingine, ingawa inafungana na Kagera Sugar.

Bossou alisema kwamba licha ya washambuliaji wengi kuongea sana kuwa watawapita na kuifunga timu hiyo, lakini wanashindwa kuonyesha uimara wao pale wanapokutana nao.

“Kwa sasa hapa Bongo sijaona mshambuliaji ambaye anaweza kunitisha wala kunifanya nimuwaze kukutana naye kwa sababu wote nawaona wa kawaida na wengi wao wanaongea na tunapokutana nao wanakuwa na viwango vya kawaida tofauti na wanavyoongea.

“Angalia hata katika mchezo uliopita yule Mavugo wa Simba, alitamba kwamba atatufunga lakini cha ajabu tulimdhibiti kirahisi tofauti na tulivyofikiria kwamba tungepata ushindani kutoka kwake na kila mtu aliona jinsi ambavyo tulifanikiwa kazi yetu.


“Labda atokee straika wa nje ndiyo anaweza kutusumbua lakini siyo hawa wa ndani ambao wengi wako kawaida sana,” alisema Bossou.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV