October 26, 2016



KRC Genk anayochezea Mbwana Samatta imekutana na kipigo katika Ligi Kuu ya Ubelgiji baada ya kuchapwa mabao 2-1 ikiwa ugenini,leo.

Sporting Charleoi ndiyo iliyoiangusha Genk licha ya Samatta kuanza.

Genk walianza kupata bao katika dakika ya 3 kupitia Nikos Karelis lakini dakika ya 11, wenyeji wakasawazisha kupitia Sotiris Ninis.

Samatta alilambwa kadi ya njano katika dakika ya 29 ya mchezo huo.

Bao 1-1 ilikwenda hadi mapumziko na kipindi cha pili mechi ilikuwa ngumu na ilikuwa vigumu kubashiri nani atashinda.

Huku ikionekana kama mechi itaisha kwa sare, Cristophe Diandy akaumaliza mchezo zikiwa zimebaki dakika nane kwa kuifungia Sporting Charleroi bao la pili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic