October 29, 2016


Watani Yanga na Simba wanakutana leo chini ya usimamizi wa Mjumbe wa Heshima wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Said El Maamry.

El Maamry anakutana na pande hizo mbili kujadili suala la beki Hassan Kessy ambaye Simba inamlalamikia kusajili Yanga huku akijua ana mkataba na Simba.

“Kweli El Maamry amekubali na Jumamosi (leo), ndiyo tunakutana kwa ajili ya kulimaliza suala hilo na Simba,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga kutoka makao makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam.

 “Lengo letu ni kulimaliza hili suala, kwa kuwa hii nafasi ya El Maamry ni nzuri kwa maana hiyo ya kulimaliza, tunaamini tutafikia mwafaka.”

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ambayo inashughulikia suala hilo, ilitoa nafasi kwa Yanga na Simba kufikia mwafaka kabla yenyewe haijatoa maamuzi.

Lakini kama Yanga itashindwa na kuamliwa kulipa, itakuwa tatizo kwao kwa kuwa tayari imeshamtumia Kessy katika mechi kadhaa za ligi.

Baada ya kamati hiyo kukaa na kupata maamuzi, iliona inawezekana pia Yanga na Simba kukutana na kulimaliza suala hilo badala ya kutoa maamuzi ambayo yatakuwa yanauumiza upande mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic