Kocha George Lwandamina raia wa Zambia, yuko jijini Dar es Salaam.
Taarifa zimeeleza kwamba kocha huyo ametua mchana na amewekwa katika moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam, Yanga wakitaka kufanya siri kubwa.
Kamati ya Ufundi ya Yanga, imempendekeza kocha huyo kutua nchini na kuinoa Yanga badala ya Kocha Hans van der Pluijm.
Hata hivyo, taarifa nyingine zimeeleza kocha huyo anaweza kuchukua nafasi ya Pluijm ambaye atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga.
Bado kumekuwa na mkanganyiko kuhusiana na kocha huyo kwa kuwa Yanga wamefanya ni siri kubwa.
Lakini habari za uhakika zimeeleza, tayari Yanga wamemalizana naye licha ya kuwa wanafanya siri kubwa kuhusiana naye.
"Kila kitu kimemalizika, kocha yuko Dar es Salaam, mambo yanakwenda safi kabisa. Lakini vuteni subira," alisema mpasha taarifa.
Lwandami alikuwa kocha bora wa Zambia msimu wa 2014-15, pia aliwahi kuinoa Zesco ya Zambia kwa mafanikio makubwa, pia timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo.
0 COMMENTS:
Post a Comment