October 3, 2016


Kocha Rogasian Kaijage ametishia kuachia ngazi kuinoa Toto Africa ya Mwanza.

Toto imekutana na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ndanda FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo.

Baada ya mechi, mashabiki wa Toto Africa walianza kumshambulia Kaijage kwa maneno ya kashfa.

“Kweli nimehuzunishwa sana, ukiangalia ligi ndiyo iko mwanzoni. Bado tunapambana na tunafanya kila kinachowezekana ili tufanikiwe.


“Mashabiki wetu wananishambulia, utafikiri mimi nina tatizo au mimi ni mtu mbaya, nimesikitishwa sana,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV