October 3, 2016Beki wa zamani wa Liverpool na West Ham United, Rigobert Song yu taabani akishambuliwa na ugonjwa wa kupooza.

Song ameanguka ghafla nyumbani kwake mjini Younde kwao Cameroon na sasa kwa mujibu wa gazeti la L’Equipe la Ufaransa, hali yake si nzuri na yu taabani sana kwenye chumba cha watu mahututi maarufu kama ICU.


Beki huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, sasa ana umri wa miaka 40 na alikuwa ni Kocha wa timu ya taifa ya Chad.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV