KIKOSI CHA COASTAL UNION MSIMU ULIOPITA |
Mashabiki wa Coastal Union wameendeleza mtindo wao wa kutoa vichapo kwa waamuzi wanaowaona 'wameiuma' timu yao.
Mashabiki wamemvamia mwamuzi wa mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya KMC FC ya Dar es Salaam na kumtwanga vibaya wakimchangia kama mpira.
Mwamuzi huyo alishindwa kujitetea na hakukuwa na msaada kwa kuwa kulikuwa na askari mmoja tu kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, hadi hapo baadaye polisi walipifika uwanjani hapo kuongeza nguvu.
Jazba za kumpiga hadi kwa mawe na kumjeruhi mwamuzi Thomas Mkombozi kutoka kilimanjaro zilitokana na Coastal Union kulambishwa mchanga kwa kuchapwa mabao 3-2 na wageni wa KMC FC.
Mshambuliaji Joseph John aliiyefungia KMC FC mabao mawili katika dakika ya 2 na 83, moja likiwa limefungwa na Rashidi Roshwa kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 89.
Mabao ya wenyeji Coastal Unioun yaliwekwa kimiani na Bakari Nendo na Seif Mkenza katika dakika za 52 na 72.
0 COMMENTS:
Post a Comment