October 11, 2016


Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amemtaka mshambuliaji wake, Ame Ali kuongeza juhudi ili apate nafasi.

Omog amemueleza Ame pamoja wachezaji wengine ambao hawapati nafasi mara kwa mara, kwamba ni kuongeza juhudi na kulenga kuisaidia timu.

“Kocha kasema kila mmoja atapata nafasi, lakini lazima kujituma na kila atakayesaidia timu ndiyo anakuwa muhimu,” kilieleza chanzo.

“Unajua wako wachezaji hawapati nafasi ya kutosha. Lakini kweli kwenye kikosi chetu ushindani upo juu sana. Naungana na kocha badala ya kulaumu, ni kujituma tu.”

Omog amekuwa ni kati ya makocha wanaoshikilia sana suala la nidhamu, pia anapenda kuwa na kikosi chenye ushindani kuanzia ndani.


Ame ambaye ametua akitokea Azam FC, bado hajapata nafasi ya kutosha kuitumikia Simba ambayo analazimika kuwapiku wageni Laudit Mavugo kutoka Burundi na Frederic Blagnon wa Ivory Coast ambao wamekuwa wakibadilishana nafasi ya washambuliaji wa kati.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV