October 17, 2016



Pamoja na kupata sare ya bao 0-0 dhidi ya Yanga, uongozi wa Azam FC umesema bado una imani na benchi lao la ufundi chini ya Kocha Mhispania, Zeben Hernandez.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema, kikosi chao kilicheza vizuri na kupoteza nafasi nyingi.

“Tunaamini kuna mambo ambayo yanawezekana, bado benchi la ufundi lina nafasi ya kurekebisha mambo.

“Hivyo tunawapa nafasi waendelee kufanya kazi na kukipanga kikosi kwa kuwa ligi ndiyo iko mwanzo,” alisema.


Azam FC ilicheza soka la kibabe zaidi katika mechi dhidi ya Yanga ambayo ilimalizika kwa sare hiyo ya bila mabao kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic